PETER RWEIKIZA THADEO1
11 April 2018 

UTANGULIZI

Kuna utofauti mkubwa wa kimantiki na kiathari kisheria kufanya bishara kwa aina mojawapo ya mifumo ya biashara iliyopo, na mantiki au athari hizi sio tu zinawakabili wafanyabiashara bali pia zinamkabili yeyote anayejihusisha na bishara hiyo, iwe mamlaka ya kiserikali, awe muajiriwa, mtoa huduma, mshirika au mteja. 

Hii ni kwasababu, aina yoyote ya mfumo wa biashara una faida na hasara zake, lakini zaidi ya hapo kila aina ya mfumo wa biashara una mantiki na athari tofauti unapoangaliwa kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo za kodi, uwezo wa kurithi au kuhamisha umiliki, kwenye madai, na kwenywe sheria na taratibu za uendeshaji aina hiyo ya mfumo wa biashara. 

Sheria kuu zinazotawala aina tofauti za umiliki wa biashara Tanzania ni: !! Sheria ya Makampuni namba 212 ya mwaka 2002 !! Sheria ya Mikataba namba 345 kama ilivyopitiwa upya mwaka 2002 !! Sheria ya usajili wa Majina ya Biashara namba 213 kama ilivyopitiwa upya mwaka 2002 AINA TOFAUTI ZA UMILIKI WA BIASHARA Kuna aina kuu tatu za mifumo ya biashara au umiliki wa biashara Tanzania ambazo ni: 

1.! Biashara ya Mtu Binafsi
2.! Biashara ya Ushirikiano 
3.!Kampuni BIASHARA YA MTU BINAFSI (SOLE TRADER) Huu ndio mfumo rahisi sana wa kufanya au kumiliki biashara kuliko aina yoyote ile ya mfumo wa umiliki wa biashara kutokana na urahisi wa kuanzisha na kufunga/kuondoa umiliki wa biashara wa aina hii. Hakuna taratibu zozote za usajili zinazohitajika 1 Mwandishi ni Mwanasheria wa sheria za Biashara na Makampuni na niwakili katika kampuni ya Uwakili ya THADESON ADVOCATES iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam. Unaweza kumfuatilia Instagram @peterthadeo1. 2 kisheria au taratibu za kufuata kufunga biashara ya mtu binafsi. 

Kisheria kufanya biashara kama mtu binafsi kunamaanisha yafuatayo: !! Mtu anafanya biashara kama yeye mwenyewe na anawajibika kwa kila hatua moja ya biashara (hii inaweza kuwa unaendesha biashara kwa jina lako au unaweza ukabuni au kusajili jina lolote la biashara, lakini hata kama utabuni au kusajili jina lolote la biashara ni lazima uonyeshe sanasana kwenye karatasi/risiti za biashara hiyo kwamba mimi fulani nafanya biashara kwa jina fulani. 

Kwa mfano kama umefungua duka la chakula na kuliita MANGI SHOP, ni lazima uonyeshe kwenye nyaraka za biashara kwamba JULIUS MOSES T/A MANGI SHOP). !! Mtu mwenyewe binafsi anamiliki mali na bidhaa zote za biashara kwa jina lake mwenyewe. !! Ni rahisi kuhamisha wakati wowote kwa mtu mwingine au kurithisha mfumo wa umiliki wa biashara wa aina hii. !! 

Mfanyabiashara wa namna hii hana majukumu yoyote anayotakiwa kutimiza kwa mtu yeyote zaidi ya atakavyo yeye mwenyewe kuendesha biashara yake. !! Njia hii pia ni rahisi kwenye ulipaji wa kodi, kwakuwa unapolipa kodi yako ya mapato unakuwa umelipia na biashara pia. !! 

Laikini athari au hatari kubwa ya aina ya mfumo huu wa umilikaji biashara ni kwamba mtu mwenyewe binafsi anabeba athari, madhara na madai yote yanayoweza kutokana na biashara anayoendesha. Kwasababu kunakuwa hakuna tofauti kati ya mali za biashara na mali zake mtu binafsi na hii maana yake ni kwamba, ikitokea madai yoyote yanayohusina na uendeshaji wa biashara hiyo, kama vile kudaiwa kodi au mtu kudai fidia kutokana na madhara aliyopata kwa kutokana na biashara hiyo, mali zote alizonazo mfanyabiashara wa aina hii, ziwe zimetokana na biashara hiyo au la, zinaweza kukamatwa ili kulipa deni hilo na hata kama hana mali zaidi, basi yeye mwenyewe binafsi atawajibika au kama mtu anamdai yeye mwenyewe binafsi anaweza kukamata mali za biashara. !! 

Pamoja na urahisi na wepesi wa kuanzisha aina hii ya umiliki wa biashara, ni lazima ikitegemea na aina ya biashara kufuata 3 taratibu za sheria kwenye kuendesha biashara hiyo kama vile kupata vibali vyote kutoka mamlaka husika kama vile leseni za biashara na taratibu kulingana na aina ya biashara. 

BIASHARA YA USHIRIKIANO (PATRNERSHIP) Mtu binafsi anaweza akafikiria kuanzisha biashara au aina fulani ya biashara na angependa kushirikiana na mtu au watu wengine kuanzisha au kuendesha biashara hiyo.

Sheria ya Mikataba namba 345 R.E 2002 inaruhusu watu kuanzia wawili wenye nia moja kuungana ili kufanya biashara kwa lengo la kutengeneza faida (kifungu 191 (1)). 

Ushirikiano huu ni zao la mkataba wa kisheria, hivyo mtu yeyote ambaye anaingia kwenye biashara ya ushirikiano ni lazima awe ana sifa za kuweza kuingia mikataba kwa mujibu wa sheria. Sifa kubwa ya msingi katika biashara ya ushirikiano ni kwamba watu kuanzia wawili na wasiozidi ishirini (kifungu 463 sheria ya Makampuni) ni lazima wakubaliane kuungana ili kufanya biashara kwa nia ya kutengeneza faida na kila mshiriki mmoja anakuwa ni mwenza na muwakilishi wa mwenzake au wenzake katika biashara, hivyo basi kitendo au matendo ya mshiriki mmojawapo katika biashara ya ushirikiano yanamfunga au yanahesabiwa kuwa ni tendo au matendo ya kila mshiriki aliyeko kwenye biashara ya ushirikiano. Nia kubwa ya kuingia kwenye biashara ya ushirikiano inaweza kuwa kwa nia mojawapo kati ya hizi: !! 

Kuongeza mtaji kwa kuchangia kwenye biashara zaidi ya mtu mmoja, au !! Kutafuta mtu mwenye ujuzi, maarifa au utaalamu wa fani fulani ili aweze kuchangia ujuzi au utaalamu wake kama mmiliki na siyo muajiriwa, au !! Kukwepa kusimamia uendeshaji wa biashara hiyo na kuacha mwingine aendeshe biashara hiyo akijua ni yake pia. n.k. Aina ya Washiriki kwenye Biashara ya Ushirikiano Mshiriki kamili (typical partner) Huyu ni Yule mshirika kwenye biashara ya ushirikiano ambaye anasimamia shughuli za kila siku za biashara na amechangia mtaji kwa kuweka pesa taslimu. 

4 Mshiriki Aliyelala (silent/dormant partner) Huyu ni yule mshiriki kwenye biashara ya ushirikiano ambaye amechangia mtaji tu kwa pesa taslimu alafu hashiriki shughuli yoyote ya kuendesha biashara wala usimamizi. Mshiriki wa Mshahara (salaried partner) Huyu kisheria anaonekana kama ni mshiriki kwenye biashara ya ushirikiano ingawa anakuwa sio sehemu ya washiriki kwakuwa hakusaini mkataba wa ushirikiano zaidi anakuwa ameajiriwa, ila kwasababu anapewa nafasi kwenye utawala na anauwezo wa kusaini nyaraka za biashara hiyo. 

Mshiriki kwa lazima (partner by estoppel) Huyu anakuwa siyo mshiriki wa biashara ya ushirikiano na wala sio muajiriwa, lakini kwakupitia maneno au matendo yake mwenyewe au yeye mwenyewe anaruhusu au anakubali kutambulishwa au kutenda kama mshiriki kwenye biashara ya ushirikiano. Mtu wa namna hii sheria inamchukulia kama mshirika wa biashara ya ushirikiano kwenye kitu au tendo ambalo amejihusisha na biashara hiyo. 

Sifa Kubwa ya Biashara ya Ushirikiano Sifa za aina ya mfumo huu wa biashara hazitofautiani sana na bishara ya mtu binafsi kwa maana ya uanzishwaji wake na usajili hauhitaji kufuata taratibu ngumu kama kampuni, ni rahisi cha muhimu kuwe na makubaliano baina ya washirika jinsi ya kuendesha biashara hiyo. Jambo kubwa la tofauti katika bishara ya ushirikiano ni umiliki wa mali na uwajibikaji yanapotokea madai. 

Umiliki wa Mali Ingawa aina ya mfumo wa biashara ya ushirikiano (partnership) haipati nguvu kisheria kumiliki mali yenyewe peke yake (not separate entity), bali mali zinakuwa kwa jina la biashara lakini zinamilikiwa na washiriki wote wa biashara sawa kwa pamoja au kwa uwiano wa umiliki wa biashara hiyo.

5 Uwajibikaji wa Mshiriki Katika Madai Katika mfumo wa aina hii wa biashara ya ushirikiano, uwajibikaji kwa washiriki yanapotokea madai yoyote huwa ni kwa pamoja (jointly) na kila mmoja mmoja (severally). Hii maana yake inapotokea mshiriki mmoja wa biashara akafanya tendo (kama kwenda kinyume na mkataba au kusababisha hasara au maumivu kwa mtu mwingine) wakati akiwa kwenye kazi za biashara hiyo ya ushirikiano, uwajibikaji (liability) uenda kwa biashara yote na kwa mshiriki mmoja mmoja wa biashara hiyo ya ushirikiano. 

Hivyo upande ulioumia una uchaguzi wa kushitaki biashara, kwa maana ya washiriki wote kwa pamoja, au mshiriki yeyote mmoja kwa niaba ya wote. Hivyo hivyo ikitokea deni au kulipa fidia, mali za biashara zitatumika kulipa deni au fidia hiyo, na kama mali za biashara ya ushirikiano hazitoshi, basi mali za washiriki zitatumika kufidia sehemu iliyobaki kwa usawa au kwa uwiano wa umiliki wa biashara hiyo. 

Na kama washiriki wengine hawana mali na labda mshiriki mmoja ndio ana mali zake binafsi, bali mali za huyo mshiriki mmoja zitatumika kufidia sehemu inayodaiwa na yeye anaweza akawadai washiriki wenzake kufidia sehemu aliyowalipia. Hii inamaanisha, kama ilivyo biashara ya mtu binafsi, mfumo wa aina ya biashara ya ushirikiano haina ukomo wa uwajibikaji kwenye madai (unlimited liability). 

Haki na Wajibu wa Washiriki Kila mshiriki kwenye biashara ya ushirikiano ana haki ya: !! kunufaika kwa usawa kwenye faida inayotokana na biashara hiyo. !! Kufidiwa gharama au hasara zozote atakazopata wakati akifanya shughuli za biashara. !! Kushiriki au kupata nafasi ya uongozi kwenye biashara hiyo. !! Kukagua na kujiridhisha taarifa za mahesabu ya biashara. !! Kuamua iwapo akubali kuruhusu kuongeza washirika wa biashara au kubadili jina na kama akikataa hata kama washiriki wote wamekubali hilo haliwezi kupita (veto). 

Kila mshiriki kwenye biashara ya ushirikiano ana wajibu wa: !! Kutoa taarifa sahihi za kila jambo analofanya linalohusiana na biashara hiyo kwa washiriki wenzake. !! Kuelezea kwa wenzake namna ambavyo amenufaika au amepokea kutokana na biashara hiyo. !! Kila mshiriki ana wajibu wa kutofanya biashara au jambo ambalo litashindana na biashara hiyo. 6 Kuna aina za biashara au huduma ambazo mtu hawezi kuanzisha kama kampuni hivyo kumlazimu kufanya binafsi au kwenye ushirikiano kama huduma za ushauri mbalimbali wa kitaalamu; kwa mfano sheria, kodi n.k. 

Lakini pia kuna aina nyingine ya biashara ya ushirikiano yenye ukomo wa uwajibikaji kwenye madai (limited liability partnership (LLP)) amabapo wataalamu wa fani mbalimbali wanautumia kutoa huduma, mfumo huu ni maarufu sana nchini Uingereza, Marekani, UAE, na nyingine, lakini kwa hapa Tanzania sheria hairuhusu. 

KAMPUNI Aina nyingine ya mfumo wa kuendesha biashara ni kwa kusajili kampuni. Kampuni ni aina ya mfumo wa kufanya biashara unaundwa na mtu mmoja au muunganiko wa watu zaidi ya mmoja na au makampuni mengine kwa kuunganisha mitaji. Sababu za kuanzisha kampuni !! Kuunda biashara ambayo itajitegemea na kujitenga na mmiliki au wamiliki ili kuweza kupata ukomo wa uwajibikaji kwenye madai (limited liability). !! 

Kuunganisha mitaji ili kufikia lengo kwa umoja. !! Kupata uwezo wa kukopa ambapo haiwezekani mtu binafsi kukopa. !! Kupata uwezo wa kufanya aina za biashara ambazo zina sharti za kufanywa kwa aina ya kampuni peke yake, mfano: biashara ya bima, taasisi za fedha, n.k. Sifa za kufanya biashara kama kampuni !! Kampuni ni mtu tofauti kisheria na wamiliki wake (separate legal personality) Hivyo basi ina mamlaka kisheria kuingia mikataba kwa jina la kampuni, mambo yote utakayofanya kupitia kampuni yanahesabiwa yamefanywa na kampuni na sio wamiliki. 

Kwahiyo ni njia nzuri ya kufanya biashara bila kuguswa na mahitaji au uwajibikaji wa biashara hiyo zaidi ya faida utakayopata. Na kwakuwa kampuni ni mtu tofauti na mmiliki, mmiliki anaweza kukopesha kampuni na kudai kama mtu yeyote wa nje. 7 !! Ukomo wa uwajibikaji kwenye madai kwa wamiliki (limited liability) Sifa nyingine kubwa ya kampuni ni uwezo wa kuwakinga wamiliki na uwajibikaji kwenye madai au madeni ya biashara. 

Hivyo basi wamiliki wa biashara ikitokea kuna madai au deni watawajibika tu kwa kiwango cha uhakikisho (guarantee) au umiliki (hisa) alizotoa kwenye kampuni ambazo hazijalipiwa na kama amelipa hisa zote hataguswa na dai au deni lolote. Hivyo basi ni mali tu za kampuni zitakazotumika kulipia hayo madai na madeni na kama zitaisha au hazitoshi basi itakuwa ndio mwisho wa kampuni lakini mdai hawezi kuvuka kugusa mali za wamiliki au mmiliki wa kampuni. !! 

Uwezo wa kuuza hisa: hii inawezekana hasa kwa aina ya makampuni ya umma. !! Uwezo wa kukasimu madaraka; ambapo wakurugenzi wanakasimu uendeshaji wa kila siku wa kampuni kwa watu walioajiriwa kuongoza kampuni (CEO). !! Kuendelea kudumu hata wamiliki wakifa (perpetual succession): sifa kubwa ya kampuni ni uwezo wa kudumu na kuendelea hata mmiliki au wamiliki wanapokufa kwakuwa kampuni ni mtu tofauti na wamiliki, ambapo hisa za mmiliki zinarithiwa. !! 

Uwezo wa kumiliki mali: kampuni ina uwezo kisheria wa kumiliki mali kwa jina lake, pia inaweza kununua na kuuza itakavyo. !! Kampuni inaweza kushitaki au kushitakiwa kwa jina lake nje ya wamiliki. Matendo yote inayofanya kampuni ni matendo ya kampuni na hayaathiri wamiliki ndio maana inaweza kushitaki au kushitakiwa peke yake. !! Kampuni ikishaanzishwa inaweza kufutwa kwa utaratibu wa sheria peke yake. 

Aina za Makampuni Tanzania 1.!Kampuni Binafsi Haya ndio aina za makampuni mengi nchini ambayo yanamilikiwa na watu binafsi, kisheria kuanzia mtu mmoja mpaka ukomo wa watu hamsini wanaweza kuanzisha kampuni 

2.!Kampuni za Umma Hii ni kampuni iliyo wazi ambayo inaweza kuanzishwa kuanzia watu wawili na haina ukomo. Hizi ndio kampuni 8 ambazo zinauza hisa zake kwa jamii na zinasajiliwa soko la hisa la Dar es Salaam. 

3.!Makampuni ya Kigeni Haya ni makampuni yote yaliyoanzishwa nje ya nchi ambayo yanataka kufanya biashara Tanzania au kuanzisha matawi ya kampuni zao Tanzania. Hata kama kampuni inamilikiwa na watanzania, lakini kama imesajiliwa nje ikija kufanya kazi Tanzania inakuwa kampuni ya kigeni. 

4.!Makampuni (Mashirika) ya Serikali Haya ni makampuni yote ya Umma ambayo serikali ina hisa zaidi ya asilimia 50 au inamilikiwa na kuendeshwa na serikali. 

Kwa mfano: TANESCO, DAWASCO, TTCL n.k. USAJILI WA KAMPUNI Ili kuweza kusajili kampuni Tanzania chini ya Sheria ya Makampuni namba 212 ya mwaka 2002, unahitaji yafuatayo: !! JINA !! MEMORANDUM OF ASSOCIATION !! ARTICLES OF ASSOCIATION !! KUJAZA FORM NO. 14a (taarifa za wakurugenzi na ofisi ya kampuni) !! KUJAZA FORM NO. 14b (fomu ya kuonyesha kampuni imetimiza masharti yote) !! KWASILISHA FOMU NA KULIPA BRELA !! KUPATA HATI YA USAJILI ZIADA Kuna aina nyingine za mfumo unaoweza kutumika kuendesha biashara hasahasa zinazojihusisha na kutoa huduma kama mashule, hospitali, makanisa, huduma mbalimbali, n.k. Aina za mifumo hiyo inajumuisha: !! Vyama vya Kijamii (civil socities and Institutes) 

Hivi vyama vinasajiliwa chini ya Sheria ya Vyama vya Kijamii namba 337 kama ilivyopitiwa upya mwaka 2002, usajili unaofanywa katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi. !! Vyama visivyo vya kiserikali (NGO’s) Kwa sasa NGO’s zinaweza kusajiliwa na kufanya biashara ili kupata mapato ya kuendesha shughuli zake. NGO’s zinaweza kusajiliwa kama Kampuni yenye ukomo wa uhakiki (limited by guarantee) chini ya sheria ya Makampuni, kama 9 chama chini ya sheria ya Vyama vya Kijamii (Societies Act), kama Trust chini ya sheria ya kusajili Trust Tanzania, au NGO chini ya sheria ya vyama visivyo vya kiserikali.